1 Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu,Ukayasikilize maneno yangu yote.
2 Tazama basi, nimefunua kinywa changu,Ulimi wangu umenena kinywani mwangu.
3 Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu;Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu.
4 Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5 Kwamba waweza, nijibu;Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.