15 Katika ndoto, katika maono ya usiku,Usingizi mzito uwajiliapo watu,Katika usingizi kitandani;
16 Ndipo huyafunua masikio ya watu,Na kuyatia muhuri mafundisho yao,
17 Ili amwondoe mtu katika makusudio yake,Na kumfichia mtu kiburi;
18 Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni,Na uhai wake usiangamie kwa upanga.
19 Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake,Na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake;
20 Hata roho yake huchukia chakula,Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.
21 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.