21 Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane;Na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje.
22 Naam, nafsi yake inakaribia shimoni,Na uhai wake unakaribia waangamizi.
23 Kwamba akiwapo malaika pamoja naye,Mkalimani, mmoja katika elfu,Ili kumwonyesha binadamu hayo yampasayo;
24 Ndipo amwoneapo rehema, na kusema,Mwokoe asishuke shimoni;Mimi nimeuona ukombozi.
25 Nyama ya mwili wake itakuwa laini kuliko ya mtoto;Huzirudia siku za ujana wake;
26 Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;Hata auone uso wake kwa furaha;Naye humrejezea mtu haki yake.
27 Yeye huimba mbele ya watu, na kusema,Mimi nimefanya dhambi, na kuyapotosha hayo yaliyoelekea,Wala sikulipizwa jambo hilo;