30 Ili kurudisha roho yake itoke shimoni,Ili atiwe mwanga kwa mwanga wa walio hai.
31 Angalia sana, Ee Ayubu, unisikilize;Nyamaza, mimi nitasema.
32 Kama una neno la kusema, nijibu;Nena, kwani nataka kukuhesabia kuwa na haki.
33 Kama sivyo, unisikilize mimi;Nyamaza, nami nitakufunza hekima.