4 Roho ya Mungu imeniumba,Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
5 Kwamba waweza, nijibu;Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame.
6 Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe;Mimi nami nilifinyangwa katika udongo.
7 Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe,Wala sitakulemea kwa uzito.
8 Hakika umenena masikioni mwangu,Nami nimesikia sauti ya maneno yako, ukisema,
9 Mimi ni safi, sina makosa;Sina hatia, wala hapana uovu ndani yangu;
10 Tazama, yuaona sababu za kufarakana nami,Hunihesabu kuwa ni adui yake;