20 Hufa ghafula, hata usiku wa manane;Watu hutikisika na kwenda zao,Nao mashujaa huondolewa pasipo mkono wa mtu.
21 Kwani macho yake ya juu ya njia za mtu,Naye huiona miendo yake yote.
22 Hapana weusi, wala hilo giza tupu,Wawezapo kujificha watendao udhalimu.
23 Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi,ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.
24 Yeye huwavunja-vunja mashujaa pasina kuwachunguza,Na kuwaweka wengine mahali pao.
25 Kwa sababu hiyo yeye huyatafiti matendo yao;Naye huwapindia usiku, wakaangamia.
26 Yeye huwapiga kama watu wabayaWaziwazi mbele ya macho ya wengine;