22 Hapana weusi, wala hilo giza tupu,Wawezapo kujificha watendao udhalimu.
23 Kwani yeye hana haja ya kumfikiria mtu zaidi,ili aende mbele za Mungu ahukumiwe.
24 Yeye huwavunja-vunja mashujaa pasina kuwachunguza,Na kuwaweka wengine mahali pao.
25 Kwa sababu hiyo yeye huyatafiti matendo yao;Naye huwapindia usiku, wakaangamia.
26 Yeye huwapiga kama watu wabayaWaziwazi mbele ya macho ya wengine;
27 Kwa sababu walikengeuka, wasimwandame yeye,Wasikubali kuzishika njia zake hata moja;
28 Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikilia,Naye akasikia kilio cha hao wateswao.