3 Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno,Kama vile kaakaa lionjavyo chakula.
4 Na tujichagulie yaliyo ya uelekevu;Na tujue wenyewe yaliyo mema.
5 Kwani Ayubu amesema, Mimi ni mwenye haki,Naye Mungu ameniondolea haki yangu;
6 Nijapokuwa mwenye haki, nimehesabiwa kuwa mwongo;Jeraha yangu haiponyeki, nijapokuwa sina makosa.
7 Je! Ni mtu gani mfano wa Ayubu,Anywaye mzaha kama maji?
8 Atembeaye na hao watendao uovu,Na kwenda pamoja na watu wabaya.
9 Kwa kuwa amenena, Haimfai mtu lo loteKujifurahisha na Mungu.