34 Watu walio na akili wataniambia,Naam, kila mtu mwenye hekima anisikiaye;
35 Huyo Ayubu amesema pasipo maarifa,Na maneno yake hayana hekima.
36 Laiti Ayubu angejaribiwa hata mwisho,Kwa kuwa amejibu kama watu waovu.
37 Kwani huongeza uasi juu ya dhambi zake,Apiga makofi kati yetu,Na kuongeza maneno yake kinyume cha Mungu.