1 Tena Elihu akajibu na kusema,
2 Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako,Au je! Wasema, Haki yangu ni zaidi kuliko ya Mungu,
3 Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe?Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?
4 Mimi nitakujibu,Na hawa wenzio pamoja nawe.