13 Hakika Mungu hatasikia ubatili,Wala Mwenyezi hatauangalia.
14 Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!
15 Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake,Wala hauangalii sana unyeti;
16 Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili;Huongeza maneno pasipo maarifa.