Ayu.
Sura 35:9-15
Swahili Union Version
9 Kwa sababu ya wingi wa jeuri wao hulia;Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.
10 Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu,Awapaye nyimbo wakati wa usiku;
11 Atufundishaye zaidi ya hayawani wa nchi,Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege za angani?
12 Hulia huko, lakini hapana ajibuye,Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.
13Hakika Mungu hatasikia ubatili,Wala Mwenyezi hatauangalia.
14Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,Hiyo daawa i mbele yake, nawe wamngojea!
15Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujilia katika hasira zake,Wala hauangalii sana unyeti;