1 Tena Elihu akaendelea na kusema,
2 Ningojee kidogo nami nitakueleza;Kwa kuwa nikali na maneno kwa ajili ya Mungu.
3 Nitayaleta maarifa yangu kutoka mbali,Nami nitampa haki Muumba wangu.
4 Kwani yakini maneno yangu si ya uongo;Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
5 Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote;Ana uweza katika nguvu za fahamu.
6 Hauhifadhi uhai wa waovu;Lakini huwapa wateswao haki yao.
7 Yeye hawaondolei macho yake wenye haki;Lakini pamoja na wafalme huwawekaKatika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.