Ayu.
Sura 36:11-17
Swahili Union Version
11 Kama wakisikia na kumtumikia,Watapisha siku zao katika kufanikiwa,Na miaka yao katika furaha.
12Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga,Nao watakufa pasipo maarifa.
13Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasiraHawalilii msaada hapo awafungapo.
14Wao hufa wakali vijana,Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.
15Yeye humponya aliyetaabika kwa njia ya taabu yake,Na kuyafunua masikio yao kwa maonevu.
16Naam, yeye angekuongoza utoke katika msibaHata mahali penye nafasi, ambapo hapana msonge;Na kilichowekwa mezani pako kingejaa mafuta.
17Lakini umejaa hukumu ya waovu;Hukumu na haki hukushika.