19 Je! Mali yako yatatosha, hata usiwe katika taabu,Au uwezo wote wa nguvu zako?
20 Usiutamani usiku,Wakati watu wakatwapo katika mahali pao.
21 Jitunze, usiutazame uovu;Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.
22 Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake;Ni nani afundishaye kama yeye?
23 Ni nani aliyemwagiza njia yake?Au ni nani awezaye kusema, Wewe umetenda yasiyo haki?
24 Kumbuka kuitukuza kazi yake,Watu waliyoiimbia.
25 Wanadamu wote wameitazama;Watu huiangalia kwa mbali