24 Kumbuka kuitukuza kazi yake,Watu waliyoiimbia.
25 Wanadamu wote wameitazama;Watu huiangalia kwa mbali
26 Tazama, Mungu ni mkuu, nasi hatumjui;Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27 Kwani yeye huvuta juu matone ya maji,Yamwagikayo katika mvua kutoka kungeni mwake;
28 Ambayo mawingu yainyeshaNa kudondoza juu ya wanadamu kwa wingi.
29 Naam, mtu aweza kuelewa na matandazo ya mawingu,Ngurumo za makao yake?
30 Tazama, yeye huutandaza mwanga wake, umzunguke;Naye hufunika vilindi vya bahari.