Ayu.
Sura 36:4-10
Swahili Union Version
4Kwani yakini maneno yangu si ya uongo;Aliyekamilika katika maarifa yu pamoja nawe.
5Tazama, Mungu ni hodari, wala hamdharau mtu ye yote;Ana uweza katika nguvu za fahamu.
6Hauhifadhi uhai wa waovu;Lakini huwapa wateswao haki yao.
7 Yeye hawaondolei macho yake wenye haki;Lakini pamoja na wafalme huwawekaKatika viti vya enzi milele, nao hutukuzwa.
8 Nao wakifungwa kwa pingu,Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;
9Ndipo huwaonyesha matendo yao,Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.
10Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo,Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.