8 Nao wakifungwa kwa pingu,Wakitwaliwa kwa kamba za mateso;
9 Ndipo huwaonyesha matendo yao,Na makosa yao, ya kuwa wametenda kwa kujivuna.
10 Yeye huyafunua masikio yao, wasikie maonyo,Na kuwaagiza warudi kuuacha uovu.
11 Kama wakisikia na kumtumikia,Watapisha siku zao katika kufanikiwa,Na miaka yao katika furaha.
12 Lakini wasiposikia, wataangamia kwa upanga,Nao watakufa pasipo maarifa.
13 Lakini hao wasiomcha Mungu mioyoni hujiwekea hasiraHawalilii msaada hapo awafungapo.
14 Wao hufa wakali vijana,Na uhai wao huangamia katikati ya wachafu.