1 Moyo wangu hunitetema kwayo pia,Nao hutoka mahali pake.
2 Zisikizeni hizo kelele za sauti yake,Na uvumi utokao kinywani mwake.
3 Yeye huituma iende chini ya mbingu zote,Na radi yake hata miisho ya nchi.
4 Baadaye sauti hunguruma;Yeye hunguruma kwa sauti ya ukuu wake;Hazizuii hapo sauti yake isikiwapo.
5 Mungu hunguruma kwa kustaajabisha kwa sauti yake;Hufanya mambo makuu, ambayo hatuwezi kuelewa nayo.