10 Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu;Na upana wa maji huganda.
11 Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji;Hulitandika wingu la umeme wake;
12 Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,Ili yafanye yote atakayoyaagizaJuu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;
13 Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake,Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.
14 Sikiliza neno hili, Ee Ayubu;Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.
15 Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza,Na kuumulikisha umeme wa wingu lake?
16 Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa,Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?