12 Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,Ili yafanye yote atakayoyaagizaJuu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;
13 Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake,Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.
14 Sikiliza neno hili, Ee Ayubu;Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.
15 Je! Wajua wewe jinsi Mungu anavyoziagiza,Na kuumulikisha umeme wa wingu lake?
16 Je! Wajua jinsi mawingu yalivyowekwa sawasawa,Hizo kazi za ajabu za huyo mkamilifu wa maarifa?
17 Jinsi nguo zako zilivyo na moto,Hapo nchi ituliapo kwa sababu ya upepo wa kusini?
18 Je! Waweza kuzitandaza mbingu pamoja naye,Ambazo zina nguvu kama kioo cha kuyeyushwa?