20 Je! Aambiwe kwamba nataka kunena?Au mtu angetamani kumezwa?
21 Na sasa watu hawawezi kuutazama mwanga ung’aao mbinguni;Lakini upepo ukipita huzitakasa.
22 Kaskazini hutokea umemetufu wa dhahabu;Mungu huvikwa ukuu utishao.
23 yeye Mwenyezi hamwezi kumwona;Yeye ni mkuu mwenye uweza;Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.
24 Kwa hiyo watu humwogopa;Yeye hawaangalii walio na hekima mioyoni.