6 Kwani huiambia theluji, Anguka juu ya nchi;Na vivyo manyonyota ya mvua,Na hayo maji ya mvua yake kubwa.
7 Huufunga mkono wa kila binadamu;Ili watu wote aliowaumba wajue.
8 Hapo wanyama huingia mafichoni,Na kukaa katika mapango yao.
9 Dhoruba hutoka katika vyumba vyake;Na baridi ghalani mwake.
10 Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu;Na upana wa maji huganda.
11 Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji;Hulitandika wingu la umeme wake;
12 Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,Ili yafanye yote atakayoyaagizaJuu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;