8 Hapo wanyama huingia mafichoni,Na kukaa katika mapango yao.
9 Dhoruba hutoka katika vyumba vyake;Na baridi ghalani mwake.
10 Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu;Na upana wa maji huganda.
11 Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji;Hulitandika wingu la umeme wake;
12 Nalo hugeuzwa huku na huku kwa uongozi wake,Ili yafanye yote atakayoyaagizaJuu ya uso wa dunia hii ikaayo watu;
13 Kama ni kwa kuonya, au kama ni kwa nchi yake,Au kama ni kwa rehema, ndiye aletaye.
14 Sikiliza neno hili, Ee Ayubu;Simama kimya, uzifikiri kazi za Mungu za ajabu.