1 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
2 Ni nani huyu atiaye mashauri gizaKwa maneno yasiyo na maarifa?
3 Basi jifunge viuno kama mwanamume,Maana nitakuuliza neno, nawe niambie.
4 Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi?Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu.
5 Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua?Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake?
6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?