14 Hubadilika mfano wa udongo chini ya muhuri,Vitu vyote vinatokea kama mavazi.
15 Na waovu nuru yao huzuiliwa isiwafikie,Na mkono ulioinuka huvunjika.
16 Je! Umeziingia chemchemi za bahari,Au umetembea mahali pa siri pa vilindi?
17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti,Au umeyaona malango ya kuzimu?
18 Umeyafahamu mapana ya dunia?Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru?Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake,Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?