17 Je! Umefunuliwa malango ya mauti,Au umeyaona malango ya kuzimu?
18 Umeyafahamu mapana ya dunia?Haya! Sema, ikiwa unayajua hayo yote.
19 Iko wapi njia ya kuyafikia makao ya nuru?Na giza pia, mahali pake ni wapi?
20 Upate kuipeleka hata mpaka wake,Upate kuelewa na mapito ya kuiendea nyumba yake?
21 Hukosi unajua, maana ulizaliwa wakati huo,Na hesabu ya siku zako ni kubwa!
22 Je! Umeziingia ghala za theluji,Au umeziona ghala za mvua ya mawe,
23 Nilizoziweka akiba kwa wakati wa misiba,Kwa siku ya mapigano na vita?