6 Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani?Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni,
7 Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja,Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?
8 Au ni nani aliyeifunga bahari kwa milango,Hapo ilipofurika kana kwamba imetoka tumboni.
9 Nilipolifanya wingu kuwa vazi lake,Na giza zito kuwa nguo ya kuifungia,
10 Nikaiagiza amri yangu;Nikaiwekea makomeo na milango,
11 Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita,Na hapa mawimbi yako yanyetayo yatazuiliwa?
12 Je! Umeiamuru asubuhi tangu siku zako zilipoanza?Umeyajulisha mapambazuko mahali pake?