1 Je! Wajua majira ya kuzaa kwao mbuzi-mwitu walio majabalini?Au waweza kusema majira ya kuzaa kulungu?
2 Je! Waweza kuhesabu miezi yao watakayoitimiza?Au je! Wajua majira ya kuzaa kwao?
3 Wao hujiinamisha, kuzaa watoto wao,Watupa taabu zao.
4 Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi;Huenda zao, wala hawarudi tena.
5 Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru?Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu?
6 Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake,Na nchi ya chumvi kuwa makao yake.