10 Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani?Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?
11 Je! Utamtumaini kwa sababu ana nguvu nyingi?Au, utamwachia yeye kazi yako?
12 Je! Utamtumaini kwamba ataileta mbegu yako nyumbani.Na kukusanya nafaka ya kiwanja chako cha kupuria?
13 Bawa la mbuni hufurahi;Lakini mabawa yake na manyoya yake, je! Yana huruma?
14 Kwani yeye huyaacha mayai yake juu ya nchi,Na kuyatia moto mchangani,
15 Na kusahau kwamba yumkini mguu kuyavunja,Au mnyama wa mwitu kuyakanyaga.
16 yeye huyafanyia ukali makinda yake, kana kwamba si yake;Ijapokuwa taabu yake ni ya bure, hana hofu;