18 Wakati anapojiinua juu aende,Humdharau farasi na mwenye kumpanda.
19 Je! Wewe ulimpa farasi uwezo wake?Au, ni wewe uliyemvika shingo yake manyoya yatetemayo?
20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige?Fahari ya mlio wake hutisha.
21 Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake;Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha.
22 Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai;Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga.
23 Podo humpigia makelele,Mkuki ung’aao na fumo.
24 Huimeza nchi kwa ukali wake na ghadhabu;Wala hasimami kwa sauti ya baragumu.