20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige?Fahari ya mlio wake hutisha.
21 Hupara-para bondeni, na kuzifurahia nguvu zake;Hutoka kwenda kukutana na wenye silaha.
22 Yeye hufanyia kicho dhihaka, wala hashangai;Wala hageuki kurudi nyuma mbele ya upanga.
23 Podo humpigia makelele,Mkuki ung’aao na fumo.
24 Huimeza nchi kwa ukali wake na ghadhabu;Wala hasimami kwa sauti ya baragumu.
25 Kila ipigwapo baragumu yeye husema, Aha!Naye husikia harufu ya vita toka mbali,Mshindo wa maakida, na makelele.
26 Je! Mwewe huruka juu kwa akili zako,Na kuyanyosha mabawa yake kwenda kusini?