4 Watoto wao wa katika hali nzuri, hukua katika bara wazi;Huenda zao, wala hawarudi tena.
5 Ni nani aliyempeleka punda-milia aende huru?Au je! Ni nani aliyemfungulia vifungo punda-mwitu?
6 Ambaye nimeifanya nyika kuwa nyumba yake,Na nchi ya chumvi kuwa makao yake.
7 Yeye hudharau mshindo wa mji,Wala hasikii kelele zake msimamizi.
8 Upana wa milima ni malisho yake,Hutafuta-tafuta kila kitu kilicho kibichi.
9 Je! Nyati atakubali kukutumikia?Au atakaa katika zizi lako?
10 Je! Waweza kumfunga nyati kwa kamba matutani?Au, yeye atayalima mabonde nyuma yako?