1 Ndipo huyo Elifazi, Mtemani, akajibu na kusema,
2 Mtu akijaribu kuzungumza nawe, je! Utaona ni vibaya?Lakini ni nani awezaye kujizuia asinene?
3 Tazama, wewe umewafunza watu wengi,Nawe umeitia nguvu mikono iliyokuwa minyonge.
4 Maneno yako yamemtegemeza huyo aliyekuwa anaanguka,Nawe umeyaimarisha magoti manyonge.
5 Lakini sasa haya yamekufikilia wewe, nawe wafa moyo;Yamekugusa, nawe wafadhaika.