12 Basi, nililetewa neno kwa siri,Sikio langu likasikia manong’ono yake.
13 Katika mawazo yaliyotoka katika maono ya usiku,Hapo usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu.
14 Hofu iliniangukia na kutetema,Iliyoitetemesha mifupa yangu yote.
15 Ndipo pepo ilipita mbele ya uso wangu;Na nywele za mwili wangu zilisimama.
16 Hiyo pepo ilisimama kimya, nisiweze kutambua sura zake,Mfano ulikuwa mbele ya macho yangu;Kulikuwa kimya, nami nilisikia sauti, ikinena,
17 Je! Binadamu atakuwa na haki kuliko Mungu?Je! Mtu atakuwa safi kuliko Muumba wake?
18 Tazama, yeye hawategemei watumishi wake;Na malaika zake huwahesabia upuzi;