6 Je! Dini yako siyo mataraja yako,Na matumaini yako si huo uelekevu wa njia zako?
7 Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia?Au hao waelekevu, walikatiliwa mbali wapi?
8 Kama mimi nilivyoona, hao walimao maovu,Na kupanda madhara, huvuna yayo hayo.
9 Kwa pumzi za Mungu huangamia.Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.
10 Kunguruma kwake simba, na sauti ya simba mkali,Na meno ya simba wachanga, yamevunjika.
11 Simba mzee huangamia kwa kukosa mawindo,Nao watoto wa simba mke wametawanyika mbalimbali.
12 Basi, nililetewa neno kwa siri,Sikio langu likasikia manong’ono yake.