1 BWANA akafuliza kumjibu Ayubu, na kusema,
2 Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi?Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.
3 Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,
4 Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini?Naweka mkono wangu kinywani pangu.
5 Nimenena mara moja, nami sitajibu;Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.