Ayu.
Sura 40:13-19
Swahili Union Version
13Wafiche mavumbini pamoja,Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.
14Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako,Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.
15Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;Yeye hula nyasi kama vile ng’ombe,
16Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake,Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.
17Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
19Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.