16 Tazama basi, nguvu zake ni katika viuno vyake,Na uwezo wake u katika mishipa ya tumbo lake.
17 Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18 Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
19 Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.
20 Hakika milima humtolea chakula;Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.
21 Hulala chini ya miti yenye vivuli,Mafichoni penye mianzi, na matopeni.
22 Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao;Mierebi ya vijito humzunguka.