Ayu.
Sura 40:17-23
Swahili Union Version
17Yeye hutikisa mkia wake mfano wa mwerezi;Mishipa ya mapaja yake yanaungamana pamoja.
18Mifupa yake ni kama mirija ya shaba;Mbavu zake ni kama vipande vya chuma.
19Yeye ni mkuu wa njia za Mungu;Yeye aliyemfanya alimpa upanga wake.
20 Hakika milima humtolea chakula;Hapo wachezapo wanyama wote wa barani.
21Hulala chini ya miti yenye vivuli,Mafichoni penye mianzi, na matopeni.
22Hiyo miti yenye vivuli humfunika kwa vivuli vyao;Mierebi ya vijito humzunguka.
23 Tazama, mto ukifurika, yeye hatetemeki;Hujiona yu salama, ijapokuwa Yordani hufurika hata kinywani pake.