2 Je! Mwenye hoja atashindana na Mwenyezi?Mwenye kujadiliana na Mungu, na ajibu yeye.
3 Ndipo Ayubu akamjibu Mungu, na kusema,
4 Tazama, mimi si kitu kabisa, nikujibu nini?Naweka mkono wangu kinywani pangu.
5 Nimenena mara moja, nami sitajibu;Naam, nimenena mara mbili, lakini sitaendelea zaidi.
6 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
7 Jifunge viuno kama mwanamume,Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.
8 Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha?Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?