6 Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema,
7 Jifunge viuno kama mwanamume,Mimi nitakuuliza neno, nawe niambie.
8 Je! Hata hukumu yangu utaibatilisha?Utanitia mimi hatiani, upate kuhesabiwa haki?
9 Au je! Wewe una mkono kama Mungu?Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?
10 Haya! Jivike sasa fahari na ukuu;Jipambe heshima na enzi.
11 Mwaga mafuriko ya hasira zako,Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.
12 Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe,Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.