9 Au je! Wewe una mkono kama Mungu?Waweza kutoa ngurumo kwa sauti kama yeye?
10 Haya! Jivike sasa fahari na ukuu;Jipambe heshima na enzi.
11 Mwaga mafuriko ya hasira zako,Ukamtazame kila mtu mwenye kiburi, ukamdhili.
12 Mtazame kila mtu mwenye kiburi ukamshushe,Ukawakanyage waovu hapo wasimamapo.
13 Wafiche mavumbini pamoja,Wafunge nyuso zao mahali palipositirika.
14 Ndipo mimi nami nitazikiri habari zako,Ya kuwa mkono wako wa kuume waweza kukuokoa.
15 Mwangalie huyo kiboko, niliyemwumba pamoja nawe;Yeye hula nyasi kama vile ng’ombe,