22 Katika shingo yake hukaa nguvu,Na utisho hucheza mbele yake.
23 Manofu ya nyama yake hushikamana;Yanakazana juu yake; hayawezi kuondolewa.
24 Moyo wake una imara kama jiwe;Naam, imara kama jiwe la chini la kusagia.
25 Anapojiinua, mashujaa huogopa;Kwa sababu ya woga wao huvunjwa moyo.
26 Mtu akimpiga kwa upanga, haumwingii;Wala fumo, wala mshale, wala mkuki wenye ncha.
27 Yeye huona chuma kuwa kama nyasi,Na shaba kama mti uliooza.
28 Mshale hauwezi kumkimbiza;Na mawe ya teo kwake hugeuka kuwa kama makapi.