4 Je! Atafanya agano pamoja nawe,Umtwae kuwa mtumishi wako milele?
5 Je! Utamchezea kama ndege?Au, kumfunga kwa ajili ya wasichana wako?
6 Je! Vikosi vya wavuvi watamfanyia biashara?Watamgawanya kati ya wafanyao biashara?
7 Je! Waweza kuijaza ngozi yake na vyuma vyenye ncha,Au kichwa chake kwa vyusa?
8 Mwekee mkono wako;Vikumbuke vile vita, wala usifanye tena.
9 Tazama, kumtamani ni bure;Je! Hatambwaga chini huyo atakayemtazama?
10 Hapana aliye mkali hata akathubutu kumwamsha;Bali ni nani awezaye kusimama mbele yangu mimi?