1 Ndipo Ayubu akamjibu BWANA, na kusema.
2 Najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote,Na ya kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika.
3 Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa?Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu,Mambo ya ajabu ya kunishinda mimi, nisiyoyajua.
4 Sikiliza, nakusihi, nami nitanena;Nitakuuliza neno, nawe niambie.