1 Haya, ita sasa; je! Yuko atakayekujibu?Nawe utamwelekea yupi katika hao watakatifu?
2 Kwani hasira humwua mtu mpumbavu,Nao wivu humwua mjinga.
3 Nimewaona wapumbavu wakishusha mizizi;Lakini mara niliyalaani maskani yake.
4 Watoto wake wako mbali na wokovu,Nao wamesongwa langoni,Wala hapana atakayewaponya.
5 Mavuno yake wale wenye njaa huyala,Na kuyatwaa hata kuyatoa miibani,Nao wenye kiu huzitwetea mali zao.
6 Kwani taabu haitoki mchangani,Wala mashaka hayachipuki katika nchi;