15 Lakini yeye huokoa na upanga wa kinywa chao,Hata kumwokoa mhitaji na mkono wake aliye hodari.
16 Basi hivi huyo maskini ana matumaini,Na uovu hufumba kinywa chake.
17 Tazama, yu heri mtu yule Mungu amwadhibuye;Kwa hiyo usidharau kurudiwa na huyo Mwenyezi.
18 Kwani yeye huumiza, lakini tena huuguza;Yeye hutia jeraha, na mikono yake huponya.
19 Yeye atakuokoa na mateso sita;Naam, hata katika saba hapana uovu utakaokugusa.
20 Wakati wa njaa atakukomboa na mauti;Na vitani atakukomboa na nguvu za upanga.
21 Utafichwa na mapigo ya ulimi;Wala usiogope maangamizo yatakapokuja.