23 Kwani utakuwa na mapatano na mawe ya bara;Nao wanyama wa bara watakuwa na amani kwako.
24 Nawe utajua ya kwamba hema yako ina salama;Na zizi lako utaliaua, wala usikose kitu.
25 Tena utajua ya kwamba uzao wako utakuwa mwingi,Na vizazi vyako watakuwa kama nyasi za nchi.
26 Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu,Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.
27 Tazama, haya tumeyapeleleza, ndivyo yalivyo;Yasikie, uyajue, ili upate mema.