6 Kwani taabu haitoki mchangani,Wala mashaka hayachipuki katika nchi;
7 Lakini mwanadamu huzaliwa ili apate mashaka,Kama cheche za moto zirukavyo juu.
8 Lakini mimi ningemtafuta Mungu,Ningemwekea Mungu daawa yangu;
9 Yeye afanyaye mambo makuu, yasiyotambulikana;Mambo ya ajabu yasiyo na hesabu;
10 Yeye atoaye mvua inyeshe juu ya nchi,Na kuyapeleka maji mashambani;
11 Awainuaye juu hao walio chini;Na hao waombolezao hukuzwa wawe salama.
12 Yeye huyatangua mashauri ya wadanganyifu,Mikono yao isipate kuyatimiza makusudi yao.